20 Machi 2025 - 17:31
Source: Parstoday
Baqaei alaani hujuma za kijeshi dhidi ya Yemen na mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani kuendelea mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya Yemen na mauaji ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.

Esmail Baqaei leo Alhamisi ametaja kuendelea mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya Yemen na kuuliwa kikatili raia wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza kuwa ni jinai za kichokozi na kivita na kusisitiza kuwa: 'Kutochukua hatua Baraza la Usalama la UN na taasisi nyingine za kimataifa mkabala wa jinai za Israel ni fedheha na haikubaliki.'

IRNA imeripoti kuwa, Esmail Baqaei ameeleza masikitiko yake makubwa kufuatia kuuliwa shahidi raia wakiwemo wanawake na watoto wasio na hatia na kubomolewa miundomsingi muhimu  huko Yemen kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na kusema kuwa hujuma zote hizi ni jinai za kivamizi na pia za kivita. Amekosoa kimya cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa mbele ya jinai za Israel na Marekani na kusema kuwa ni aibu na jambo lisilokubalika. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria kuuliwa kwa umati mamia ya wanawake na watoto wa Kipalestina kufuatia mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza siku kadhaa zilizopita na kusema: 'Wale wote wanaouhami na kuuunga mkono utawala wa Kizayuni kwa silaha, fedha na kisiasa  ni washirika wa jinai za utawala huo.'

Amesema, sambamba na kujiri mashambuliz ya anga ya Marekani dhidi ya Yemen ambayo yalianza katka duru ya utawala wa chama cha Democrat chini ya uongozi wa Rais Joe Biden; kwa kuongezeka maangamizi ya kizazi huko Gaza hakuna shaka yoyote inayosalia kwamba Marekani na Wazayuni wanatekeleza njama ya pamoja  lengo likiwa ni kuudhofisha Umma wa Kiislamu na kuzima wito wowote wa kushikamana na kuwahami wananchi madhulumu wa Palestina. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha